WATU BINAFSI NA BAADHI YA TAASISI ZA URUSI ZAWEKEWA VIKWAZO NA MAREKANI.
Marekani imewawekea vikwazo watu binafsi na
taasisi kadhaa za Urusi kwa tuhuma za kuingilia uchaguzi wa Marekani pamoja na
mashambulizi ya mtandaoni.
Alama muhmu za marekani. |
Hata hivyo vikwazo hivyo havikuwagusa maafisa
wa serikali ambao wapo karibu na Rais Vladimir Putin, na kusababisha wabunge wa
pande zote mbili za vyama vikuu nchini Marekani kusema kwamba Rais Donald Trump
anahitaji kuchukua hatua zaidi.
Wakati Marekani ikiwa chini ya shinikizo kubwa,
hatua zilizotangazwa na Wizara ya Fedha ni za kwanza muhimu kuwahi kuchukuliwa
dhidi ya nchi hiyo tokea Trump kuingia madarakani Januari 2017.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Ryabkov alisema kwamba Urusi inaandaa
hatua za kulipiza kisasi, huku uhusiano kati ya nchi hizo mbili ukionekana
kuharibika tena.
WATU BINAFSI NA BAADHI YA TAASISI ZA URUSI ZAWEKEWA VIKWAZO NA MAREKANI.
Reviewed by safina radio
on
March 16, 2018
Rating:
No comments