TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO TEHAMA YASAIDIA MAHAKAMA
Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha
Jaji Sekela Moshi amesema kuwa utaratibu wa kutumia Teknolokia ya Habari na
Mawasiliano TEHAMA katika mahakama umesaidia kuweka takwimu za mwenendo wa kesi
katika mahakama nyingi na hivyo kurahisisha utoaji wa hukumu.
JAJI SEKELA MOSHI. |
Akifunga mafunzo kwa majaji sitini na moja kutoka
kwa mahakama kuu kanda zote hapa nchini yaliyofanyika jijini Arusha Jaji Moshi
amesema kuwa utaratibu wa kutumia TEHAMA katika kutoa hukumu umeonyesha matokeo
chanya hasa katika mahakama ya biashara na vitengo vingine vya mahakama kuu
jambo ambalo wataliendeleza.
Aidha, Jaji Moshi amesema kuwa takwimu za kimahakama
kwa sasa ziko vizuri katika mfumo huo TEHAMA kutokana na kuwa unarahisisha
katika upatikanaji wake kwa kuwa takwimu zisipopangiliwa vizuri inasababisha utoaji
wa haki usiwe mzuri.
Kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu na Mkuu wa Chuo
cha Uongozi wa Mahakama ya Lushoto EJA ambacho kimetoa mafunzo hayo kwa
ufadhili wa Benki Kuu ya Dunia Dk. Paul Kiwelu amesema kuwa watatoa mafunzo
zaidi kwa majaji kwani bado kuna uhitaji mkubwa wa teknolojia hiyo.
TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO TEHAMA YASAIDIA MAHAKAMA
Reviewed by safina radio
on
March 29, 2018
Rating:
No comments