BI. ANGELA MERKEL AMEAPISHWA BUNGENI MJINI BERLIN KUWA KANSELA WA UJERUMA KUONGOZA TENA KWA MUHULA WA NNE.


BERLIN.

Angela Merkel ameapishwa bungeni mjini Berlin kuwa Kansela wa Ujerumani kuongoza tena kwa muhula wa nne.

Image result for Angela Merkel
Angela Merkel.
Bi Merkel amekula kiapo leo mbele ya spika wa bunge na aliyekuwa waziri wa fedha Wolfgang Shoubo.

Awali, Merkel alichaguliwa na bunge la Ujerumani -Bundestag, kwa kura 364 kati ya 688 katika raundi ya kwanza ya upigaji kura ambapo Merkel alihitaji kushinda kura zisizopungua 355 katika bunge hilo lenye viti 709.

Aidha habari zinaeleza kuwa kulikuwa na kura karibu 315 za kupigwa zinazomwezesha Markel kuchaguliwa tena huku wabunge tisa wakijizuia kupiga kura.

Kwa mara ya kwanza mume wa Merkel Joackim Seuya alihudhuria shughuli hiyo ya upigaji kura pamoja na mama yake Halindi Kasna
Aidha, mawaziri 15 wa serikali ya Merkel waliapishwa hapo bungeni.

BI. ANGELA MERKEL AMEAPISHWA BUNGENI MJINI BERLIN KUWA KANSELA WA UJERUMA KUONGOZA TENA KWA MUHULA WA NNE. BI. ANGELA MERKEL AMEAPISHWA BUNGENI MJINI BERLIN KUWA KANSELA WA UJERUMA KUONGOZA TENA KWA MUHULA WA NNE. Reviewed by safina radio on March 14, 2018 Rating: 5

No comments