ZFDA YATEKETEZA KWA MOTO KILO 48 ZA NYAMA KUTOKA AFRIKA KUSINI.


ZANZIBAR.

Mamlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar ZFDA imeteketeza kwa moto kilo arobaini na nane za nyama kutoka Afrika Kusini zilizoingizwa nchni kinyume cha sheria ambazo zinazosadikika kuwa na virusi vinavyo sababisha ugonjwa wa MISTERIA.

Image result for Mkuu wa Kitengo cha Utambuzi wa Hatari zinazotokana na chakula wa ZFDA Aisha Suleiman
Mkuu wa kitengo cha Uchambuzi wa hatari zinazotokana na Chakula kutoka Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar ZFDA Aisha Suleiman Akizungumza na Wandishi wa Habari.

Mkuu wa Kitengo cha Utambuzi wa Hatari zinazotokana na chakula wa ZFDA Aisha Suleiman amesema kuwa nyama hiyo iliyokuwa mali ya Kampuni ya Kamar ya Vingunguti jijini Dar es salaam ilikamatwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume visiwani Zanzibar wiki iliyopita.

Aidha, amefafanua kuwa uamuzi wa kuteketezwa kwa nyama hiyo ni kutokana na marufuku iliyopitishwa na Mamlaka hiyo ya uingizwaji wa nyama, maziwa na samaki kutoka Afrika Kusini ambapo ugonjwa MISTERIA umesababisha vifo vya watu mia moja themanini mpaka sasa.

Hivi karibuni Malmlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar imekabidhiwa cheti cha mfumo wa uhakiki ubora wa huduma cha kiwango cha kimataifa cha IFO ikiwa ni kielelezo cha Mamlaka hiyo kusimamia misingi ya ubora wa huduma katika kiwango cha kimataifa.

ZFDA YATEKETEZA KWA MOTO KILO 48 ZA NYAMA KUTOKA AFRIKA KUSINI. ZFDA YATEKETEZA KWA MOTO KILO 48 ZA NYAMA KUTOKA AFRIKA KUSINI. Reviewed by safina radio on March 14, 2018 Rating: 5

No comments