TANZANIA YAAHIDI KUFANYA MAPITIO YA SERA ZAKE ZA NDANI ILI KULINDA MASOKO YA NDANI NA BIDHAA ZINAZOZALISHWA.


Serikali imesema kuwa inaunga mkono makubalino ya kuundwa soko huru la pamoja barani Afrika ingawa itakuwa makini katika kuangalia maeneo yaliyoanishwa kushirikiana ili kulinda maslahi ya soko lake na bidhaa mbali mbali zinazozalishwa nchini.

Image result for UMOJA WA AFRIKA.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa baada ya kutia saini makubaliano ya kuanzishwa soko huru la pamoja katika mkutano wa Umoja wa Afrika uliomalizika jana katika mji wa Kigali nchini Rwanda.

Image result for waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa tanzania mh. majaliwa kassim majaliwa

Aidha, Mh. Majaliwa amesema kuwa mbali na kusainiwa makubaliano hayo kuna manufaa kwa serikali hivyo inabidi kurudi nchini kukaa katika baraza la mawaziri kuungana na wanasheria ili kufanya mapitio kwa maeneo ambayo Tanzania inaweza kupata makwazo kutokana na sheria zilizopo nchini.

Pia, amesema kuwa kuangalia na mapitio hayo yatakayofanyika nchini yatasaidia katika kupata namna ya kuendeleza uchumi kutoka uchumi wa chini hadi kufikia uchumi wa kati.

Hatua ya kusainiwa makubaliano hayo ni ishiri ya kuleta matumaini kwa inchi za Afrika kuwa ndoto ya waasisi wa Afrika katiika kushirikiana katika Nyanja za kiuchumi sasa inaelekea kutimia licha ya kuwepo kwa baadhi ya mataifa kuomba muda wa kumalizia.


TANZANIA YAAHIDI KUFANYA MAPITIO YA SERA ZAKE ZA NDANI ILI KULINDA MASOKO YA NDANI NA BIDHAA ZINAZOZALISHWA. TANZANIA YAAHIDI KUFANYA MAPITIO YA SERA ZAKE ZA NDANI ILI KULINDA MASOKO YA NDANI NA BIDHAA ZINAZOZALISHWA. Reviewed by safina radio on March 22, 2018 Rating: 5

No comments