KAMISHENI YA KISWAHILI YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI YAKABILI NA CHANGAMOTO YA FEDHA
Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili katika
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Prof. Keneth Simala amesema Kamisheni ya
Nchi hizo zinakabiliwa na changamoto ya rasilimali fedha katika majukumu yake
ya kukuza lugha ya Kiswahili ambayo kwa sasa inazungumzwa na watu zaidi ya
milioni 200 duniani.
Prof. Simala ameyasema hayo katika mkutano wa wadau wa
nchi wanachama pamoja na vyama vya kitaifa na kikanada vya kukuza lugha ya
Kiswahili kilichofanyika jijini Arusha kujadili changamoto zinazowakabili.
Aidha, Prof. Simala amewaomba wananchi kushirki
katika kutoa mawazo hususani wanaojihusisha na masuala ya Kiswahili katika
tafiti zinazofanywa na kamisheni hiyo ili kufahamu changamoto na mahitaji yao.
Mmoja wa wadau wa lugha hiyo Kenny Waibora amesema
kuwa katika kukuza Kiswahili inapaswa viongozi wanachama wa nchi hiyo kutumia
lugha ya Kiswahili katika mikutano wanapoalikwa kuhutubia.
KAMISHENI YA KISWAHILI YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI YAKABILI NA CHANGAMOTO YA FEDHA
Reviewed by safina radio
on
March 27, 2018
Rating:
No comments