TRUMP AJIANDAA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA SEKTA YA TEKNOLOJIA NA MAWASILIANO YA CHINA.
WASHINGTON.
Rais
wa Marekani Donald Trump anajiandaa kuchukua hatua dhidi ya sekta ya
tekinolojia na mawasiliano nchini China ikiwemo kuongezwa kwa viwango vya kodi
kwa bidhaa zinavyoagizwa nchini humo.
Rais wa Marekani Donald Trump. |
Wiki
iliyopita maafisa wa ngazi ya juu wanaohusika na masuala ya biashara nchini
humo waliwasilisha kwa Rais Trump mpango unaohusisha viwango vikubwa vya kodi.
Habari
zinaeleza kuwa kiasi ya dola bilioni 30 zinatarajiwa kukusanywa kutokana na
ushuru utakaotozwa kwa bidhaa zinazohusiana na sekta ya tekinolojia na
mawasiliano zinazoingizwa nchini Marekani kutoka China.
Aidha,
hatua hiyo inakuja wakati Marekani ikiyatuhumu makampuni ya kitekinolojia ya
nchini China ambayo yamekuwa yakiyataka makampuni ya Marekani kutoa siri zake
za kitekinolojia kabla ya kuruhusiwa kuendesha shughuli zao nchini humo.
Hata
hivyo, Mwenyekiti wa kamati inayohusika na masuala ya kodi katika baraza la
wawakilishi, Kevin Brady amewaambia waandishi wa habari kuwa rais Trump
amedhamiria kupambana dhidi ya tuhuma hizo za wizi wa kitekinolojia.
TRUMP AJIANDAA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA SEKTA YA TEKNOLOJIA NA MAWASILIANO YA CHINA.
Reviewed by safina radio
on
March 14, 2018
Rating:
No comments