HALMASHAURI NA MIKOA ZATAKIWA KUTENGA FUNGU KWA AJILI YA KITENGO CHA HABARI, JAFFO.
ARUSHA.
Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na
serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh Suleman
Jaffo ameagiza mikoa na halmashauri zote nchini kutenga fungu kwaajili ya
kitengo cha habari ikiwa ni pamoja na
kuwaruhusu maafisa habari kuingia katika vikao vyote vya maamuzi ili waweza
kutoa habari sahihi kwa umma.
Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh Suleman Jaffo. |
Waziri Jafo ameyasema hayo mapema leo wakati
akifunga kikao kazi cha 14 cha maafisa habari,mawasiliano na mahusiano
serikalini kilichomalizika leo mkoani
Arusha.
Aidha Mh Jaffo amesema kuwa ipo mikoa na halmashauri
ambazo haziwaruhushu maafisa habari kuingia katika vikao vya maamuzi kwa
kukwepa baadhi ya taarifa kujulikana kwa umma ambapo waziri huyo amesema kuwa
atahakikisha suala hilo linafanyiwa kazi ili kuondoa maswali mengi kwa wanachi
dhidi ya majukumu yanayofanywa na serikali.
Waziri huyo pia mewataka wakuu wote wa idara na
vitengo kuwapa takwimu sahihi maafisa habari ili waweze kuzitoa katika tovuti
za halmashauri ili serikali pamoja na wananchi waweze kupata taarifa za
maendeleo
HALMASHAURI NA MIKOA ZATAKIWA KUTENGA FUNGU KWA AJILI YA KITENGO CHA HABARI, JAFFO.
Reviewed by safina radio
on
March 16, 2018
Rating:
No comments