UMOJA WA MATAIFA WAUNGA MKONO UCHAGUZI MPYA NCHINI ZIMBABWE
Umoja wa mataifa umetangaza kuunga mkono uchaguzi mpya
unaoandaliwa kufanyika mwezi Julai nchini Zimbabwe na kuitaka serikali ya taifa
hilo kutoa kipaumbele cha dharura kwa uchumi wa taifa hilo.
Achim Steiner |
Achim Steiner, kiongozi wa mpango wa maendeleo katika umoja wa
mataifa UNDP alikuwa ziarani jijini Harare na kukutana na raisi Emmerson
Mnangagwa.
Steiner amesema Umoja wa mataifa unaendelea kuunga mkono
mchakato wa maandalizi ya uchaguzi na jitihada za kuinua uchumi.
Uchaguzi wa uraisi unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi
August ambapo Mnangagwa atakabiliwa na ushindani tangu alipochukua madaraka
kutoka kwa aliyekuwa kiongozi mkongwe wa taifa hilo Robert Mugabe, ambaye
alijiuzulu mwezi Novemba baada ya kutawala kwa takribani miongo minne.
UMOJA WA MATAIFA WAUNGA MKONO UCHAGUZI MPYA NCHINI ZIMBABWE
Reviewed by safina radio
on
March 19, 2018
Rating:
No comments