MZAZI YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUMSHAWISHI MTOTO WAKE KUANDIKA MAJIBU YA UONGO KATIKA MITIHANI HATUA KALI ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE, MTAKA.


SIMIYU.

Mkuu wa Mkoa wa Simuyu Anthon Mtaka amesema kuwa mzazi yeyote atakayebainika kumshawishi mtoto wake kuandika majibu yasiyosahihi katika mtihani wa kitaifa wa darasa la saba ili asifaulu kuandelea na masomo ya kidato cha kwanza hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Image result for Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka
Mkuu wa Mkoa wa Simuyu Anthon Mtaka.
Mtaka ametoa kauli hiyo katika kikao cha wadau wa elimu wilayani Maswa kilichokutanisha kamati za shule, na ushirikiano wa wazazi na walimu pamoja na wadau mbali mbali wa elimu.

Aidha, amekemea tabia ya baadhi ya wazazi kuwataka watoto wao kuandika majibu yasiyo sahihi ili wasifaulu huku akiwashangaa kwa jambo hilo kwa kuwa wamekuwa wakijitolea katika kutekeleza ujenzi wa miradi ya kielimu ikiwemo mabomba ya maji pamoja na kuchangia michango mbali mbali.

Katika kiakao hicho shule mbali mbali zilizofanya vizuri katika mtihani wa kitaifa wa darasa la saba wamepewa motisha ya majiko ya gesi na vyeti vya kutambua mchango wao.

MZAZI YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUMSHAWISHI MTOTO WAKE KUANDIKA MAJIBU YA UONGO KATIKA MITIHANI HATUA KALI ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE, MTAKA. MZAZI YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUMSHAWISHI MTOTO WAKE KUANDIKA MAJIBU YA UONGO KATIKA MITIHANI HATUA KALI ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE, MTAKA. Reviewed by safina radio on March 15, 2018 Rating: 5

No comments