Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe amesema kuondoka kwake ofisini mwezi Novemba mwaka jana kulikuwa ni mapinduzi
Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe amesema
kuondoka kwake ofisini mwezi Novemba mwaka jana kulikuwa ni mapinduzi ya
kijeshi na kutoa wito wa hali hiyo kubadilishwa.
RAIS MUGABE |
Mugabe ametoa kauli hii kwenye mahojiano yake ya kwanza ya
televisheni tangu ang’olewe madarakani na nafasi yake kuchukuliwa na rais wa
sasa Emmerson Mnangagwa.
Aidha, Mugabe amesisitiza kuwa kilichofanyika ni mapinduzi ya
kijeshi na kudai kuwa mrithi wake rais Mnangagwa asingeweza kuwa rais wa taifa
hilo kama asingepata msaada wa jeshi.
Kauli ya Mugabe imekuja wakati huu wanaharakati kadhaa wakienda
Mahakama ya Katiba kutaka kubatilishwa kwa namna rais Mnangagwa alivyoingia
madarakani wakisema alitumia jeshi kupindua Serikali halali.
Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe amesema kuondoka kwake ofisini mwezi Novemba mwaka jana kulikuwa ni mapinduzi
Reviewed by safina radio
on
March 16, 2018
Rating:
No comments