JESHI LA SAUDIA ARABIA LAANGUSHA MAKOMBORA SABA


Jeshi la anga la Saudi Arabia limeyaangusha makombora saba yaliyofyatuliwa siku ya jumapili kutoka Yemen na wapiganaji wa Kihouthi.

Image result for PICHA YA MAKOMBORA

Kwa mujibu wa msemaji wa muungano wa majeshi unaoongozwa na Saudi Arabia, Kanali Turki al-Malki, mtu mmoja ameuawa baada ya kuangukiwa na mabaki ya makombora hayo, na wawili wamejeruhiwa.

Taarifa ya Saudi Arabia na washirika wake katika vita hivyo ambavyo vimedumu kwa miaka mitatu nchini Yemen, imeeleza kuwa majeshi ya Saudi Arabia yaliyazuia makombora matatu kaskazini mashariki mwa mji wa Riyadh, saa chache tu kabla ya usiku wa manane wa kuamkia leo.

Aidha makombora yaliyorushwa katika miji ya kusini mwa Najran, Jizan na Khamis Mushait pia yaliharibiwa.

Shambulizi hilo ni la tatu katika muda wa miezi mitano ambapo makombora yamerushwa mjini Riyadh huku Wahouthi wakiimarisha hatua za kuonesha wanaweza kuushambulia mji mkuu wa Saudi Arabia, hatua inayotishia kuzidisha uhasama katika kanda hiyo kati ya Iran na Saudi Arabia.

JESHI LA SAUDIA ARABIA LAANGUSHA MAKOMBORA SABA JESHI LA SAUDIA ARABIA LAANGUSHA MAKOMBORA SABA Reviewed by safina radio on March 26, 2018 Rating: 5

No comments