MKUU WA MKOA WA MANYARA ALEXANDER MNYETI AMEMUAGIZA MKURUGENZI WA WILAYA YA HANANG KUFUNGUA ZAHANATI YA KIJIJI CHA GANGAL


Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' Brayceson Kibasa Kufungua Zahanati ya kijiji cha Gangal ndani ya mwezi mmoja ili kuwaepushia wananchi adha ya kufuata huduma za afya kwa Umbali mrefu.


Image result for PICHA YA MKUU WA MKOA WA MANYARA ALEXANDER MNYETI
MKUU WA MKOA WA MANYARA ALEXANDER MNYETI
Mnyeti ametoa agizo hilo  baada ya kusikia kero kubwa ya wananchi hao wanaokabiliwa na hadha ya upatikanaji wa huduma za afya ambapo baadhi ya wagonjwa wanalazimika kuzifuata huduma hizo katika hospitali ya Haydom iliyopo wilaya ya Mbulu.

Amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wake wanazipata huduma muhimu kama za Afya kwa urahisi na kwa wakati muafaka ili waweze kufanya shughuli zao za maendeleo wakiwa na Afya njema

Ameongeza kuwa hakuna sababu ya wananchi hawa kuendelea kuzifuata huduma za afya kilomita 23 kwasababu jengo hilo tayari limeshakamilika na amemtaka Mkurugenzi kupeleke wahudumu wa afya ndani ya mwezi mmoja ili wananchi waweze kupata huduma bora za afya.

Awali akisoma taarifa  ya ujenzi wa zahanati hiyo, mbele ya mkuu wa
mkoa huyo Alexander Mnyeti,  Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya  hiyo Dkt.Jackoracha Daimon amesema ujenzi wa zahanati kuwa ulianza  mwaka 2013 kwa jitihada za wananchi kwa kuchangia fedha na nguvu kazi.
Dkt.Daimon alisema  ujenzi wa zahanati hiyo umegharimu jumla ya
sh.ml,65,640,000 ambapo wananchi wamechangia sh mil. 26,000,000 huku halmashauri ya Wilaya hiyo   ikiunga mkono jitihada za wananchi hao kwa kuchangia jumla ya sh.mil. 33, 640,000 kutoka mapato yake ya ndani.

MKUU WA MKOA WA MANYARA ALEXANDER MNYETI AMEMUAGIZA MKURUGENZI WA WILAYA YA HANANG KUFUNGUA ZAHANATI YA KIJIJI CHA GANGAL MKUU WA MKOA WA MANYARA ALEXANDER MNYETI AMEMUAGIZA MKURUGENZI WA WILAYA YA HANANG KUFUNGUA ZAHANATI YA KIJIJI CHA GANGAL Reviewed by safina radio on March 19, 2018 Rating: 5

No comments