SERIKALI INAKUSUDIA KULIWEZESHA SHIRIKA LA SIDO
Naibu waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya
amesema kuwa serikali inakusudia kuliwezesha shirika la SIDO ili liweze kufanya
kazi zake vizuri hapa nchini.
Naibu waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya |
Mhandisi Manyanya ameyasema hayo wakati Kamati ya kudumu ya bunge ya
viwanda,biashara na mazingira kuitaka serikali kuliwezesha kifedha shirika hilo
mkoani Iringa ili kukuza sekta ya viwanda hapa nchini.
Wakizungumza baada ya kutembelea karakana ya SIDO ya mkoa wa Iringa
wajumbe wa kamati hiyo wameonyesha kushangazwa na mashine zinazotumia
tekinolojia za zamani na nyingine zikiwa hazifanyi kazi kutokana na uchakavu.
Meneja wa Sido wa mkoa wa Iringa Francesiko Saimon Amesema kuwa shirika
hilo limeweza kutengeneza mashine mbalimbali za kukamua mafuta na kusaga
nafaka.
SERIKALI INAKUSUDIA KULIWEZESHA SHIRIKA LA SIDO
Reviewed by safina radio
on
March 20, 2018
Rating:
No comments