RAIS WA BURUNDI ATIA SAINI SHERIA TATA
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza hapo jana ametia saini sheria
tata inayotoa wito kwa wananchi wa taifa hilo wenye umri wa kupiga kura ya
maoni juu ya marekebisho ya katiba ambayo yanaweza kumruhusu kuendelea kukaa
madarakani hadi mwaka wa 2034 kushiriki kwenye kura hiyo.
RAIS WA BURUNDI PIERRE NKURUNZIZA |
Rais huyo mwenye umri wa miaka 54 ambae yupo madarakani tangu
mwaka 2005, sasa anataka kuendelea kusalia kwenye nafasi hiyo hadi mwaka 2035.
Sheria hiyo ya mabadiliko ya katiba ya Burundi inasema
mabadiliko yataidhinishwa iwapo asilimia 50 ya kura za ndio na kura moja
itafikiwa.
Hata hivyo upinzani unasema alichokifanya rais Nkurunziza
kinakwenda kinyume na katiba ya nchi, maana mabadiliko ya katiba ili
yaidhinishwe, lazima yapitie katika mabaraza ya bunge na seneti.
Hata hivyo wale wote wanaohitaji kuendesha kampeni ya ndio au
hapana kuhusu mabadiliko ya katiba wamepewa muda wa hadi April 6 kujiorodhesha
kwa tume ya uchaguzi ambapo kampeni imepangwa kuanza majuma mawili kabla ya
terehe ya kupiga kura.
RAIS WA BURUNDI ATIA SAINI SHERIA TATA
Reviewed by safina radio
on
March 19, 2018
Rating:
No comments