SUMA-JKT YAKABIDHIWA KANDARASI YA KUJENGA MABANDA YA VIWANDA LA HEKARI TATU.
DODOMA.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles
Mwijage amemkabidhi mkandarasi SUMA-JKT eneo la hekari tatu mjini Dodoma kwa lengo
la kujenga mabanda ya viwanda ili yawe mfano kwa wanaojifunza namna ya
kuanzisha viwanda vyao.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage. |
Katika Hafla ya Makabidhiano hapo jana Dk. Mwijage
amesema ni fursa kwa wajasiriamali na wananchi wengine mkoani humo kuanzisha
viwanda nchini chini ya usimamizi wa shirika la kusimamia na kuhudumia viwanda
vidogodogo SIDO.
Aidha, amesema kuwa anawatafuta watu ambao hawana
fedha wala hawafahamu lolote kuhusiana na viwanda ili kuwafundisha namna ya
kupata fedha na kujenga viwanda huku akiwahitaji watu wenye fedha na hawafahamu
namna ya kutumia fedha hizo waweze kujifunza matumizi mazuri ya fedha kwa uwekezaji
wa viwanda.
Naye, Mkurugenzi wa SIDO Prof. Silvesta Mkunduji
amesema kuwa shirika la SIDO limejipanga kuhakikisha kuwa azma ya serikali ya
kufikia uchumi wa kati na wa viwanda unatekelezwa kwa vitendo, kwa kutoa
elimu,teknolojia na mikopo kwa watanzania waliotayari kujiunga na SIDO.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa halmashauri ya Dodoma
Mjini na Naibu Waziri wa ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na watu wenye ulemavu
Anthon Mavunde ameshukuru serikali kupitia wizara yake kujenga viwanda katika
jimbo lake.
SUMA-JKT YAKABIDHIWA KANDARASI YA KUJENGA MABANDA YA VIWANDA LA HEKARI TATU.
Reviewed by safina radio
on
March 15, 2018
Rating:
No comments