MLIPUKO WA BOMU WAUA WATU 11 NCHINI SYRIA.
Mlipuko wa bomu umewaua watu 11 katika jengo
moja la ghorofa nne mjini Afrin, kaskazini mashariki mwa Syria, wakiwemo raia
saba na wapiganaji wanne, muda mfupi baada ya Uturuki kutangaza kuukomboa mji
huo kutoka kwa wapiganaji wa Kikurdi wa kundi la YPG.
Bomu
hilo ambalo linaelezwa kutegwa na magaidi, liliripuka wakati waasi wa kundi
lijiitalo Jeshi Huru la Syria wakifanya msako baada ya kufanikiwa kuwaondoa
wanamgambo wa Kikurdi na kutangaza udhibiti kamili, kufuatia wiki nane za
mapambano makali.
Wakati huo
huo, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema zaidi ya watu 6,000 wameondoka mashariki
mwa mji uliozingirwa wa Ghouta.
Hilo linatokea baada ya Rais Bashir al Assad
kufanya ziara katika eneo hilo linalowaaniwa kwa lengo la kuwapongeza wanajeshi
kwa kufanikisha hatua ya kuwaonda waasi karibu na mji mkuu wa Damascus.
MLIPUKO WA BOMU WAUA WATU 11 NCHINI SYRIA.
Reviewed by safina radio
on
March 19, 2018
Rating:
No comments