WATU 68 WAMEKUFA NCHINI VENEZUELA WALIPOJARIBU KUTOROKA JELA.
Watu 68 wamekufa nchini Venezuela wakati walipojaribu kutoroka kwenye jela
moja baada ya moto kuzuka kwenye vyumba ambavyo walikuwa wakizuiliwa na Polisi.
Mwanasheria mkuu wa Serikali Tarel William ametoa idadi hiyo usiku wa
kuamkia leo kwenye makao makuu ya polisi kaskazini mwa mji wa Carabobo, akilaumu
kuwa moto huo uliwashwa kwa makusudi.
Kwa upande wake mkuu wa gereza hulo Carlos Nieto amesema baadhi ya wafungwa
waliungua hadi kufa na wengine kwa kukosa hewa baada ya moto kuanza kuunguza
magodoro na kuanza kuiba silaha kutoka kwa walinzi wakijaribu kutoroka.
Miongoni mwa waliokufa ni wanawake wawili ambao walienda kuwatembelea ndugu
zao,na kutokana na tukio hilo waendesha mashtaka wanne wameteuliwa kuchunguza
chanzo chake.
Picha zilizopigwa na vuguvugu la Nieto limeonesha askari wa zima moto
wakijaribu kumuokoa mfungwa mmoja aliyekuwa akiungua.
Hata
hivyo wafungwa wengi nchini Venezuela wanataabika kutokana na hali mbaya za
magereza, kukosekana kwa mahitaji muhimu ya kibinadamu na jela kujaa kupita
kiasi huku wakikabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi.
WATU 68 WAMEKUFA NCHINI VENEZUELA WALIPOJARIBU KUTOROKA JELA.
Reviewed by safina radio
on
March 29, 2018
Rating:
No comments