NAIBU WAZIRI WA MALI ASILI NA UTALII MH. JAPHET HASUNGA AMESEMA SERIKALI ITAKAMILISHA UTARATIBU KUENDESHA JESHI LA USU.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Japhet Hasunga amesema kuwa serikali ipo katika hatua za mwisho katika kukamilisha utaratibu wote wa namna ya kuendesha  jeshi Usu kwa Watendaji wake wa Idara ya Maliasili kutoka mfumo wa zamani wa kiraia ambao utawawezesha watendaji kufanya kazi kwa pamoja na kwa weledi.

Image result for PICHA YA JAPHET HASUNGA NAIBU WAZIRI WA UTALII
NAIBU WAZIRI WA UTALII JAPHET HASUNGA

Mh Hasunga ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya kijeshi kwa Menejimenti, Mameneja wa Kanda na Maafisa Waandamizi wa wakala wa huduma za misitu nchini ambapo amesema kuwa serikali ipo katika hatua za mwisho katika kukamilisha utaratibu wote wa namna  ya kuendesha jeshi hilo.

Aidha amesema kuwa kutokana na utaratibu ambao wizara inayo kwa sasa ni kuhakikisha kuwa jeshi hilo litafanya kazi katika taasisi zote za wizara ambazo zinahusika na uhifadhi wa malisili za taifa zikiwemo Mamlaka ya Hifadhi Tanzani-TANAPA, Mamlaka ya Uhifadhi ya Ngorongoro-NGA.

Ameongeza kuwa utaratibu huo upo katika hatua za mwisho za kukamilishwa baada ya rais kukubali kuanzishwa kwa vyeti vilivyotayarishwa na wizara na hivyo jeshi hilo litaanzishwa mara moja.

Naye, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Nchini Prof. Dosantos Silayo amesema kuwa mfumo huo utasaidia kuleta mabadiliko katika utendaji.

NAIBU WAZIRI WA MALI ASILI NA UTALII MH. JAPHET HASUNGA AMESEMA SERIKALI ITAKAMILISHA UTARATIBU KUENDESHA JESHI LA USU. NAIBU WAZIRI WA MALI ASILI NA UTALII MH. JAPHET HASUNGA AMESEMA SERIKALI ITAKAMILISHA UTARATIBU KUENDESHA JESHI LA USU. Reviewed by safina radio on March 26, 2018 Rating: 5

No comments