UINGEREZA YATNGAZA KUFUKUZA WANADIPLOMASIA 23 WA URUSI.
LONDON.
Uingereza imetangaza leo kuwa
itawafukuza kutoka nchini humo wanadiplomasia 23 wa Urusi na kusitisha
mawasiliano ya ngazi ya juu na ikulu ya Kremlin, kuhusiana na shambulio la sumu ya kuua mishipa ya fahamu dhidi ya jasusi wa zamani wa Urusi na binti yake
nchini Uigereza.
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May. |
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amelimbia
bunge kuwa wana diplomasia hao 23, waliotambuliwa kuwa maafisa wa upelelezi
ambao hawakubainishwa, wana muda wa wiki moja kuondoka nchini humo.
Mwaliko wa waziri wa mambo ya nje
wa Urusi Sergei Lavrov pia umefutwa,huku Bi May akisema kuwa mawaziri wa
Uingereza na wanafamilia ya Kifalme hawatahudhuria mashindano ya kombe la soka
ya dunia yatakayofanyika nchini Urusi mwaka huu.
May ametangaza hatua hizo baada ya
Urusi kupuuza muda wa mwisho ulitolewa kueleza namna sumu iliyotengenezwa na
Umoja wa Kisovieti ilivyotumika dhidi ya Sergei na Yulia Skripal.
Ubalozi wa Urusi mjini London
umelaani hatua hiyo ya May na kuitaja kuwa ya uhasama, isiyokubalika, na isiyo
na mashiko.
UINGEREZA YATNGAZA KUFUKUZA WANADIPLOMASIA 23 WA URUSI.
Reviewed by safina radio
on
March 14, 2018
Rating:
No comments