Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassimu Majaliwa amesema nchi za Afrika ziunganishe nguvu.


Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassimu Majaliwa amesema kuwa nchi za Afrika zinapaswa kuunganisha nguvu ili kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.
Image result for picha ya waziri majaliwa kassim majaliwa
WAZIRI MKUU MAJALIWA
Waziri mkuu ameyasema hayo jijini Dar-es-salaam wakati akifungua mkutano wa 15 wa jumuiya ya mawaziri wa afya wa nchi za Afrika Mashariki,Kati na kusini mkutano wenye lengo la kujadili mpango wa kuunganisha nguvu ili kuboresha sekta ya afya.
Amesema kuwa pamoja na nchi hizo kupambana na magonjwa  hayo bado kuna tatizo sugu la magonjwa ya kifua kikuu,utapia mlo na magonjwa ya milipuko barani Afrika.
Kwa upande wake waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh Ummy Mwalimu amesema kuwa,Tanzania imejidhatiti kukabiliana na magonjwa hayo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya.
Naye katibu mkuu wa jumuiya hiyo Bw Yoshua Ndambisya amesema kuwa kuna umuhimu wa kuwa na sera ya pamoja ili kuzuia magonjwa yasiyoambukiza .
Hata hivyo mkutano huo una mpango wa kujadili mpango wa kuunganisha nguvu ili kuboresha sekta ya afya na  kujadili changamoto zinazokwamisha juhudi hizo.    

Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassimu Majaliwa amesema nchi za Afrika ziunganishe nguvu. Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassimu Majaliwa  amesema nchi za Afrika ziunganishe nguvu. Reviewed by safina radio on March 20, 2018 Rating: 5

No comments