POLISI WAMKAMATA MTUHUMIWA MWENYE NUYARAKA MBALI MBALI ZA SERIKALI.


DAR-ES-SALAAM.

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam linamshikilia Bw Suleman Massudi kwa tuhuma za kukutwa na nyaraka mbali mbali za serikali ikiwemo mihuri 53 ya kughushi, na vyeti feki vya chuo na taasisi za serikali.
Image result for Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa katika eneo la Yombo Kilakala baada ya jeshi hilo kupata taarifa kuwa kuna kundi la watu linalijihusisha na kutengeneza vyeti feki na mihuri.
Kamanda Mambosasa amesema kuwa miongoni mwa mihuri iliyokutwa kwa mtuhumiwa huyo ni muhuri wa baraza la taifa la mitihani Tanzania, chuo cha ufundi stadi VETA, Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Chuo cha Bandari, Chuo Kikuu Huria, Chuo Kikuu Mtwara, Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Chuo cha Usafirishaji NAT, Chuo cha usimamizi Fedha IAFM, pamoja na Chuo cha Uhasibu.

Katika hatua nyingine Kamanda Mambosasa amesema kuwa wanawashikilia wanawake watatu kwa tuhuma za kutumia jina la rais mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na familia yake kutapeli watu kwa kutumia mtandao wa kijamii wa facebook.




POLISI WAMKAMATA MTUHUMIWA MWENYE NUYARAKA MBALI MBALI ZA SERIKALI. POLISI WAMKAMATA MTUHUMIWA MWENYE NUYARAKA MBALI MBALI ZA SERIKALI. Reviewed by safina radio on March 16, 2018 Rating: 5

No comments