MKUU WA WILAYA YA ARUSHA BW. FABIAN DAQQARO AMEWATAKA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA UANDIKISHWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw Fabian Daqqaro amewataka
wakazi wa jiji la Arusha kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishwaji wa
vitambulisho vya taifa pamoja na kutoa ushirikiano kwa NIDA ili kurahisisha
zoezi hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw Fabian Daqqaro |
Bw Daqqaro ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha ambapo amesema
kuwa zoezi la uandikishaji na upataji wa vitambulisho vya taifa litasaidia katika
kupata idadi kamili kwenye matumizi ya masuala ya serikali pamoja na kuimarisha
daftari la wapiga kura.
Aidha amesema kuwa zoezi la NIDA katika Wilaya ya
Arusha limeshafanyika kwenye kata zaidi 15 ambapo kwa sasa zoezi hilo lipo
katika kata ya kati,ofisi za NIDA na ofisi za Mkuu wa Mkoa pamoja na kata ya
Muriett maeneo ya Mkonoo,Morombo na Nadosoito.
Vilevile ameeleza kuwa zoezi hilo ni la muhimu kwa
ajili ya maendeleo ya nchi katika Nyanja mbalimbali ikiwemo za kiuchumi,kisiasa
na kijamii pamoja na kupata takwimu sahihi katika kutengeneza mipango mbalimbali ya
kimaendeleo.
Hata hivyo amesema kuwa mpaka sasa tayari
wamewasambaza maafisa uhamiaji kwa kila kituo ambacho zoezi la uandikishaji
linafanyika kwa lengo la kugundua na kukamata wahamiaji haramu.
MKUU WA WILAYA YA ARUSHA BW. FABIAN DAQQARO AMEWATAKA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA UANDIKISHWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA.
Reviewed by safina radio
on
March 16, 2018
Rating:
No comments