IMEBAINISHWA KUWA MANENO MABAYA YANAWEZA KUHARIBU MFUMO WA MAISHA.


Imebainishwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa maneno mabaya yanayotamkwa juu ya mtu kupata uhalali na yakaharibu kabisa mfumo mzima wa maisha ya mtu huyo.

Image result for PICHA YA UZAO WA MZABIBU


Huduma ya redio safina kesho katika ukumbi wa maombi uliopo Mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana imekuandalia maombi maalumu ya kufuta maneno mabaya yaliyotamkwa juu watu ili wasifanikiwe katika maisha yao.

Aidha, maneno mabaya yaliyotamkwa juu ya baadhi ya watu yamekuwa  mkosi kwani husababisha kukosa kazi,wengine kushindwa kumalizia ujenzi wa nyumba, huku wengine wakishindwa kusoma kutokana na magonjwa ya mara kwa mara pamoja na kukosa ada ya masomo.  

Vile vile, kutokana na maneno mabaya yaliyotamkwa juu ya maisha yao kupata kibali yamesababisha watu kushindwa kuoa na kuolewa, kupata watoto katika ndoa zao, kuvunjika kwa mahusiano ya urafiki au uchumba hadi kusababisha migogoro katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, mtu atatatakiwa kufika kesho katika ukumbi wa maombi uliopo mbauda na kielelezo cha kitendo cha kiimani cha mzao wa mzabibu [Damu ya Yesu] kwa ajili ya kufanya kitendo cha kiimani cha kufuta maneno yote mabaya ambayo yametamkwa na adui juu ya maisha ya watu ili wasiweze kufanikiwa.

IMEBAINISHWA KUWA MANENO MABAYA YANAWEZA KUHARIBU MFUMO WA MAISHA. IMEBAINISHWA KUWA MANENO MABAYA YANAWEZA KUHARIBU MFUMO WA MAISHA. Reviewed by safina radio on March 28, 2018 Rating: 5

No comments