WANANCHI WA MISRI WANAPIGA KURA LEO KUMCHAGUA RAIS


Wananchi wa Misri wanapiga kura leo kuchagua rais kati ya rais wa sasa Abdel Fattah al-Sisi na mgombea mwingine mdogo ambaye anakabiliwa na ukosoaji mkubwa kuwa ni kibaraka wa Sisi.
Image result for PICHA YA RAIS WA MISRI ABDEL FATTAH AL-SISI
RAIS WA SASA WA MISRI ABDEL FATTAH AL -SISI
Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa majira ya saa  moja asubuhi katika zoezi litakalochukua siku tatu ambapo rais al-Sisi anatarajiwa kushinda kwa muhula wa pili wa kipindi cha miaka minne.
Usalama umeimarishwa nchi nzima kutokana na tishio la kutekelezwa mashambulizi na wapiganaji wa kiislamu wa Islamic State ambao wametishia kushambulia maeneo ya mitambo ya kupokelea matokeo na hata kwenye vituo.
Siku ya Jumamosi polisi wawili waliuawa katika shambulio la bomu kwa kutumia gari, shambulio likilenga msafara wa mkuu wa usalama kwenye jimbo la Alexandria.
Jumla ya wapiga kura milioni 60 wameandikishwa kupiga kura katika taifa ambalo asilimia kubwa raia wake ni waarabu.

WANANCHI WA MISRI WANAPIGA KURA LEO KUMCHAGUA RAIS WANANCHI WA MISRI WANAPIGA KURA LEO KUMCHAGUA RAIS Reviewed by safina radio on March 26, 2018 Rating: 5

No comments