MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH.SAMIA SULUHU AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA ROJA BOHIS KUHUSU MASUALA YA AFYA NA UCHUMI PAMOJA MAMBO MENGINE.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Roja Bohis Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Bill and Mallinda Gate Foundation mjini Dodoma na
kuafikiana dhidi ya masuala ya afya na uchumi na mambo mengine.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa
wamezungumza mambo mengi na Mkurugenzi huyo kwa masuala ya afya, uwezeshaji
wanawake kiuchumi,kilimo cha kisasa,kuongeza thamani ya mazao pamoja na masoko.
Aidha, Makamu wa Rais amezungumzia suala la
upatikanaji wa maji safi na salama hasa kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam
ambapo mara kwa mara kumekuwapo na magonjwa ya milipuko.
Kwa upande wake Roja Bohis Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Bill and Mallinda Gate Foundation ameipongeza serikali ya Tanzania
kwa hatua kubwa waliyoipiga katika kuwajumuisha wanawake katika masuala
yanayohusu fedha.
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH.SAMIA SULUHU AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA ROJA BOHIS KUHUSU MASUALA YA AFYA NA UCHUMI PAMOJA MAMBO MENGINE.
Reviewed by safina radio
on
March 23, 2018
Rating:
No comments