RAIS WA ZAMANI WA UFARANSA NICOLAS SARKOZY AHOJIWA KWA MARA YA PILI.


Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas sarkozy amerejea katika kituo cha polisi leo ili kuhojiwa kwa mara ya pili kuhusiana na madai kwamba kiongozi wa zamani wa Libya Muamar Gaddafi alimsaidia kwa fedha katika kampeni yake ya uchaguzi wa rais mwaka 2007.

Image result for RAIS SARKOZY AKIHOJIWA POLISI LEO
RAIS WA ZAMANI WA UFARANSA NICOLAS SARKOZY
Sarkozy mwenye umri wa miaka 63, aliwasili katika ofisi za maafisa wanaohusika na rushwa, utakatishaji fedha na ukwepaji kodi magharibi mwa mji wa Paris katika kitongoji cha Nanterre.

Rais huyo alikamatwa kwa mara ya kwanza jana asubuhi, lakini aliondoka kutoka katika jengo hilo la polisi usiku wa manane. Mawakili wake hawakujibu walipotakiwa kutoa maelezo.

Tangu mwaka 2013, majaji waliokuwa wanafanya uchunguzi wamekuwa wakichunguza ripoti za vyombo vya habari, pamoja na taarifa za mtoto wa gaddafi Seif al-Islam, ambazo zinadai kwamba fedha zilitolewa katika juhudi za Sarkozy kugombea urais.

RAIS WA ZAMANI WA UFARANSA NICOLAS SARKOZY AHOJIWA KWA MARA YA PILI. RAIS WA ZAMANI WA UFARANSA NICOLAS SARKOZY AHOJIWA KWA MARA YA PILI. Reviewed by safina radio on March 21, 2018 Rating: 5

No comments