WAUZA MADAWA YA KULEVYA 13 WAUAWA NA JESHI LA POLISI UFILIPINO.


Jeshi la Polisi nchini Ufilipino limewaua washukiwa 13 wa biashara haramu ya madawa ya kulevya katika operesheni iliyoendeshwa  katika mkoa wa Bulacan nchini humo.


Jeshi hilo limefahamisha kuwa limeshambuliwa na walanguzi hao wa madawa ya kulenvya na polisi kujihami na kisha kufyatua risasi nakufanikiwa kuwaua washukiwa hao 13. 
Katika tukio hilo zaidi ya watu 100 wanaoshukiwa kuhusika na biashara haramu ya madawa ya kulevya wamekamatwa.
Watu zaidi ya elfu nne wamekwisha kuuawa nchini Ufilipino wakishukiwa kuhusika na baishara ya madawa ya kulevya tangu rais Rodrigo Duterte kuchaguliwa kuwa rais wa Ufilipino.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanailaumu serikali ya Duterte yakidai kuwa inakiuka haki za binadamu.


WAUZA MADAWA YA KULEVYA 13 WAUAWA NA JESHI LA POLISI UFILIPINO. WAUZA MADAWA YA KULEVYA 13 WAUAWA NA JESHI LA POLISI UFILIPINO. Reviewed by safina radio on March 23, 2018 Rating: 5

No comments