RAIS MAGUFULI AMESEMA KUWA SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA SEKTA YA AFYA NCHINI.
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh John
Magufuli amesema kuwa serikali itaendelea kuboresha sekta ya afya kwa kuongeza
bajeti ili kuhakikisha kuwa wananchi wake wanapata huduma nzuri za afya.
RAIS MAGUFULI |
Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar-es-salaam wakati akizindua
magari 181 ya kusambaza vifaa tiba katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambayo
yametolewa na shirika la kimataifa la Global Fund.
Amesema kuwa watanzania wasipokuwa na afya njema
hawataweza kufanya kazi hasa kipindi hiki serikali inapohimiza uchumi wa
viwanda hivyo wameona ni vyema wakawekeza kwenye sekta ya afya,ambapo pia amelishukuru
shirika hilo kwa kutoa msaada huo wa magari ambayo yatarahisisha usambazaji wa
dawa katika hospitali na vituo mbalimbali vya afya hapa nchini.
Kwa upande wake waziri wa afya maendeleo ya jamii
jinsia wazee na watoto Mh Ummy Mwalimu amesema kuwa serikali ya awamu ya tano
inaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ya afya ikiwemo vituo vya afya
katika mikoa ya Geita,Kagera,Mwanza,Tanga,Simiyu,Tabora na Singida.
Naye mkurugenzi mkuu wa bohari kuu ya dawa(MSD) Bw
Lauran Bwanakunu amesema kuwa mgari hayo yaliyozinduliwa yatasaidia kuongeza
uwezo wa kusambaza vifaa tiba hadi kwenye vituo vya afya tofauti na hapo awali
ambapo usambazaji wa dawa ulikuwa unaishia hospitali za wilaya.
RAIS MAGUFULI AMESEMA KUWA SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA SEKTA YA AFYA NCHINI.
Reviewed by safina radio
on
March 26, 2018
Rating:
No comments