HUDUMA YA REDIO SAFINA KESHO IMEANDAA MAOMBI MAALUMU YA KUHITIMISHA KITENDO CHA KIMAANI CHA KUCHOVYA MIGUU KWENYE MAFUTA KWA AJILI YA KUFUNGULIWA KWENYE VIFUNGO VYA MUDA MREFU.
Imebainishwa kuwa watu wengi wamepigwa na shetani
katika maeneo mbalimbali ikiwemo elimu,uchumi,afya pamoja na karama na vipawa
baada ya watu hao kubainika kuwa ni malango ya mafanikio katika familia zao.
Huduma ya redio safina kesho katika ukumbi wa maombi
uliopo mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana
imekuandalia maombi maalumu ya hitimisho la kuchovya miguu kwenye mafuta kwa
ajili ya kufunguliwa kwenye vifungo vya muda mrefu.
Aidha kesho katika ukumbi huo kutafanyika maombi ya
ukombozi kwa wazaliwa wa kwanza kama lango kwani wengi wameshambuliwa na adui
pindi wanapo jaribu kutoa msaada kwa ndugu zao kama vile kuwasomesha,kuwapatia
huduma za matibabu,chakula na malazi au kusuluhisha migogoro ya kifamilia.
Vile vile kwa mujibu wa somo hilo malango ya mzaliwa
wa kwanza yanaposhughulikiwa au kukamatwa na adui mtu huyo hushindwa kufanya
jambo lolote la kimaendeleo katika maisha yake kutokana na shetani kuondoa
kibali cha mzaliwa huyo wa kwanza mbele ya ndugu zake pamoja na jamii kwa
ujumla.
Hata hivyo siku ya kesho kila mmoja anakumbushwa
kubeba mafuta yaliykuwa yakiombewa na watumishi wa Mungu kwa njia ya redio ili
kufanya kitendo cha imani cha kushughulikia na kufunguliwa malango ya mzaliwa
wa kwanza.
HUDUMA YA REDIO SAFINA KESHO IMEANDAA MAOMBI MAALUMU YA KUHITIMISHA KITENDO CHA KIMAANI CHA KUCHOVYA MIGUU KWENYE MAFUTA KWA AJILI YA KUFUNGULIWA KWENYE VIFUNGO VYA MUDA MREFU.
Reviewed by safina radio
on
March 23, 2018
Rating:
No comments