CHELSEA YAONDOLEWA KWENYE KLABU BINGWA ULAYA

Antonio Conte greets Lionel Messi at the final whistle.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema alihisi kwamba kichapo cha 3-0 ambacho klabu yake ilipokezwa katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano "hakikuwa cha haki".
Lionel Messi alifunga mabao mawili naye Ousmane Dembele akafunga moja - bao lake la kwanza akichezea Barca - na kuwasaidia miamba hao wa Uhispania kuondoka na ushindi wa jumla wa 4-1.
Mechi ya kwanza uwanjani Stamford Bridge ilikuwa imemalizika 1-1.
Matokeo hayo yaliwaondoa Chelsea kutoka kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu na msimu ujao wanakabiliwa na kibarua cha kufuzu kutokana na ushindani mkali kwenye nafasi nne za kwanza Ligi ya Premia.
CHELSEA YAONDOLEWA KWENYE KLABU BINGWA ULAYA CHELSEA YAONDOLEWA KWENYE KLABU BINGWA ULAYA Reviewed by safina radio on March 15, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.