KOREA KASKAZINI IKO TAYARI KUACHANA NA MPANGO WAKE WA SILAHA ZA NYUKLIA.


Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amemwambia Rais wa China Xi Jinping kwamba utawala wake uko tayari kuachana na matumizi ya silaha za nyuklia.


Image result for PICHA YA RAIS WA KOREA KASKAZINI
RAIS WA KOREA KASKAZINI KIM JONG UN
Shirika la habari la China, Xinhua limeripoti hayo leo, wakati ambapo Kim, ambaye ni mshirika wa China amefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi, kabla mikutano ya kilele na Korea Kusini na Marekani.

Kim amesema suala la kuachana na silaha za nyuklia katika Rasi ya Korea linaweza kutatuliwa, kama Korea Kusini na Marekani zitaitikia juhudi zao kwa nia njema, kuweka mazingira ya amani na utulivu, huku wakichukua hatua zaidi kwa ajili ya kupatikana kwa amani.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe amesema nchi yake inataka kupata maelezo ya kina kutoka kwa China, kuhusu mazungumzo yaliyofanyika kati ya Xi Jinping na Kim.

KOREA KASKAZINI IKO TAYARI KUACHANA NA MPANGO WAKE WA SILAHA ZA NYUKLIA. KOREA KASKAZINI IKO TAYARI KUACHANA NA MPANGO WAKE WA SILAHA ZA NYUKLIA. Reviewed by safina radio on March 28, 2018 Rating: 5

No comments