RAIS TRUMP WA MAREKANI AMESEMA ATAWEKA ADHABU KALI KWA WANAOJIHUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA.
Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa anataka kuweka adhabu kali
ikiwemo adhabu ya kifo kwa wale watakao baninika kujihusisha na biashara haramu
ya dawa za kulevya nchini humo.
RAIS TRUMP WA MAREKANI. |
Habari zinaeleza kuwa Trump anaweka adhabu hiyo lengo likiwa ni
kukabiliana na ongezeko kubwa la watumiaji wa madawa ya kulevya nchini
Marekani.
Katika hotuba yake
aliyoitoa akiwa New Hampshire,Tramp amesema kuwa wauzaji wa dawa za kulevya
wamesababisha vifo vya maelfu ya watu, lakini cha ajabu baada ya kuhukumiwa
kufungwa wamekuwa wakikaa muda mfupi tu gerezani jambo ambalo anasema haridhishwi
nalo.
Ameongeza kuwa tatizo
hilo linaweza kuondolewa kwa kutumia akili na kuwa imara pamoja na kutenga
fedha.
Rais Tramp amebainisha
kuwa yeye pamoja na bunge tayari wameafikiana kutenga kiasi cha dola billioni 6
katika bajeti mpya ya mwaka 2018/2019 ili kukabiliana na tatizo la dawa za
kulevya.
Hata hivyo Rais Trump
ameelezea mikakati iliyowekwa tayari katika kukabiliana na dawa za kulevya hadi
sasa mojawapo ikiwa ni kupunguza kiwango cha uhitaji wa dawa hizo.
Rais Trump ameahidi
kujenga taifa huru katika masuala ya matumizi ya dawa za kulevya kwa kizazi
kijacho na kuhakikisha hakuna mazingira yatakayosababisha watu kujitumbukiza
katika matumizi ya dawa za kulevya.
RAIS TRUMP WA MAREKANI AMESEMA ATAWEKA ADHABU KALI KWA WANAOJIHUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA.
Reviewed by safina radio
on
March 20, 2018
Rating:
No comments