ZAIDI YA WAPIGANAJI 18 WAUAWA NA WENGINE 13 KUJERUHIWA WA KUNDI LA TALIBAN, AFGHANNISTAN.
KABUL.
Zaidi
ya wapiganaji 18 wa kundi la Taliban wameuawa na wengine 13 kujeruhiwa kwenye
mapigano mapya dhidi ya kundi hilo katika mikoa mbalimbali nchini Afghanistan.
Kundi la Taliban la Afghanistan. |
Gavana wa wilaya ya Imam
Sahib mkoani Kunduz, kaskazini mwa nchi hiyo Mahbub Sayyedi amesema wapiganaji
wawili wa Taliban waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa baada ya vikosi vya
usalama vya Afghanistan kukabiliana na washambuliaji hao jana katika kituo cha
ukaguzi kilichoko Joy Bigam wilayani
humo.
Habari zinaeleza kuwa wizara
ya ulinzi ya Afghanistan leo imesema kuwa wapiganaji 6 wa Taliban waliuawa na
wengine 4 kujeruhiwa kwenye mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya Kajaki na
Marja, mkoani Helmand, kusini mwa nchi hiyo.
Wakati huohuo jana katika
mkoa wa Farah, magharibi mwa nchi hiyo, wapiganaji 10 wa kundi hilo waliuawa na
wengine 6 kujeruhiwa baada ya jeshi la Afghanistan kufanya mashambulizi ya anga
na operesheni ya kutokomeza kundi hilo katika wilaya ya Bala Buluk.
ZAIDI YA WAPIGANAJI 18 WAUAWA NA WENGINE 13 KUJERUHIWA WA KUNDI LA TALIBAN, AFGHANNISTAN.
Reviewed by safina radio
on
March 16, 2018
Rating:
No comments