ONGEZEKO LA USHINDANI NDANI YA EAC YAKWAMISHA MAUZO YA BIDHAA ZA KENYA.


NAIROBI.

Katibu mkuu wa Wizara ya viwanda nchini Kenya Bi Betty Maina amesema, Kenya inafanya juhudi za kuwavutia wawekezaji wa kigeni kuanzisha viwanda nchini humo ili kuongeza uuzaji wa bidhaa zake katika soko la dunia.

Image result for KENYA

Bi Maina amesema kuwa mauzo ya bidhaa za Kenya katika nchi za Afrika Mashariki yamekuwa yakikwamishwa kutokana na kuongezeka kwa ushindani,ingawa  Kenya inawatafuta wawekezaji wanaoweza kutengeneza bidhaa kwa ajili ya soko la kimataifa.

Hata hivyo amesema kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ilikuwa ni soko lenye faida kubwa kwa bidhaa za Kenya lakini sasa nchi hizo zimeanzisha viwanda ambavyo vinatengeneza bidhaa ambazo zilikuwa zinaagizwa kutoka nchini Kenya.

ONGEZEKO LA USHINDANI NDANI YA EAC YAKWAMISHA MAUZO YA BIDHAA ZA KENYA. ONGEZEKO LA USHINDANI NDANI YA EAC YAKWAMISHA MAUZO YA BIDHAA ZA KENYA. Reviewed by safina radio on March 16, 2018 Rating: 5

No comments