WATU WALIOFARIKI KWA AJALI YA MOTO NCHINI YAFIKIA 64


Serikali ya Urusi leo imesema kuwa watu waliofariki katika ajali ya moto iliotokea jana katika mji wa Siberia wa Kemerovo sasa imefikia 64.


Video for PICHA YA MOTO NCHINI URUSI


Waziri wa masuala ya dharura Vladmir Puchkov amethibitisha hayo , kufuatia moto ulioliteketeza duka moja kubwa mjini humo,ambapo watu kadhaa bado hawajulikani waliko.


Moto huo ulitokea katika jengo la ghorofa nne lenye  jina Winter Cherry umezimwa mapema leo baada ya kuwaka na kuliteketeza jengo hilo kwa muda wa saa nne.

Chanzo cha moto huo hakijajulikana,ambapo duka hilo kubwa lililofunguliwa mwaka 2013, lina maeneo ya sinema kituo cha michezo kwa watoto na bustani ya wanyama.

WATU WALIOFARIKI KWA AJALI YA MOTO NCHINI YAFIKIA 64 WATU WALIOFARIKI KWA AJALI YA MOTO NCHINI YAFIKIA 64 Reviewed by safina radio on March 26, 2018 Rating: 5

No comments