MIGUNA MIGUNA AFUKUZWA KWA MARA YA PILI NCHINI KENYA


Hatimaye mwanasisa wa upinzani nchini Kenya, Miguna Miguna, amefukuzwa kwa mara ya pili tena nchini humo baada ya hapo jana  kusafirishwa kwa ndege iliyokuwa ikielekea Canada.

Image result for PICHA YA MIGUNA MIGUNA
MIGUNA MIGUNA
Wakili wa mwanasiasa huyo amethibitisha kufukuzwa tena kwa Miguna Miguna alipozungumza na shirika lahabari la AFP.
Februari 26, Mahakama ya Juu iliwaamuru maafisa wa uhamiaji kumruhusu Miguna Miguna arejee nchini Kenya ambapo alirejea Jumatatu wiki hii.
Akizungumza kwa njia ya simu, Cliff Ombeta, mwanasheria wa Miguna, amesema mteja wake amepandishwa ndege inayoelekea Dubai lakini hawakujua ni wapi anapelekwa.

MIGUNA MIGUNA AFUKUZWA KWA MARA YA PILI NCHINI KENYA MIGUNA MIGUNA AFUKUZWA KWA MARA YA PILI NCHINI KENYA Reviewed by safina radio on March 29, 2018 Rating: 5

No comments