JAMII YATAKIWA KUWATUNZA WANYAMA IKIWA NI PAMOJA NA KUWAPATIA HUDUMA ZA AFYA
Jamii imetakiwa kutambua ya kuwa inayo mchango mkubwa
wa kuwatunza,kuwathamini na kuwalinda wanyama ikiwa ni pamoja na kuwapatia
huduma za afya.
Hayo yamesemwa na Bw,Livingstone Masija mkurugenzi
wa chama cha kutetea na kulinda ustawi wa wanyama mkoani Arusha, Arusha Society
For the Protection of Animals (ASPA) wakati akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake kuhusu umuhimu wa wananchi kuwatunza wanyama ili waweze kupata
maendeleo kupitia wanyama hao.
Aidha
amesema kuwa kutokana na mpango mkakati wa kidunia wa kupunguza umasikini
kwenye jamii kuna baadhi ya wanyama ambao wanatumika katika kufanikisha
maendeleo ya millennium akiwemo Punda hii ikiwa na lengo la kurahisisha huduma kwa
kijamii.
Ameongeza kuwa watu wote wanatakiwa kuhakikisha kuwa
wanyama wanakuwa na afya nzuri kwa kuzingatia chanjo zinazotolewa na serikali
kuu pamoja na taasisi mbalimbali zisizo kuwa za kiserikali lengo likiwa ni
kuwezesha kuwepo na huduma endelevu ya afya ya wanyama hapa nchini.
Hata hivyo chama cha ASPA, ni chama cha kutetea na
kulinda ustawi wa wanyama ambacho kilianzishwa mnamo mwaka 1997 na kushirikiana
na serikali pamoja na mashirika mengine katika kutoa elimu juu ya afya ya
wanyama.
JAMII YATAKIWA KUWATUNZA WANYAMA IKIWA NI PAMOJA NA KUWAPATIA HUDUMA ZA AFYA
Reviewed by safina radio
on
March 15, 2018
Rating:
No comments