NACTE YATANGAZA UDAHILI KWA WANAFUNZI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA NA ATASHAHADA.


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi NACTE limetangaza udahili kwa wanafunzi katika kozi za Astashahada na Stashahada katika vyuo vyenye uwezo wa kupokea wanafunzi na kutaka vyuo hivyo kutokusajili wanafunzi wasiosajiliwa na NACTE.

Image result for Mkuu wa Kitengo cha Udahili katika Baraza hilo, Twaha Twaha
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kitengo cha Udahili katika Baraza hilo, Twaha Twaha, amezitaka vyuo hivyo mara baada ya kufanya udahili wa wanafunzi kutuma majina NACTE kwa uhakiki wa sifa na vigezo vya wanafunzi hao katika kozi walizoziomba.

Aidha amesema kuwa Chuo hakitaruhusiwa kumpokea mwanafunzi yeyote ambaye haja hakikiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi-NACTE ili kumuhakikishia mwanafunzi kuwa amedahiliwa kwenye chuo kinachotambuliwa na kozi anayoisoma kuwa inatambuliwa na Baraza hilo.

Pia, amesema kuwa NACTE imeandaa mfumo mpya ujulikanao kuwa STUDENTS INFORMATION VERIFICATION SYSTEM yaani Mfumo wa Taarifa wa Utambuzi wa Wanafunzi.

Hata hivyo, Twaha amewataka wanafunzi wanaoomba udahili kuhakikisha kuwa wanaomba nafasi katika vyuo ambavyo vimeorodheshwa katika tovuti ya NACTE ambapo udahili huo umeanza tangu February 20 na utahitimishwa machi 25 mwaka huu isipokuwa katika kada ya afya kwa vyuo visivyokuwa vya serikali udahili utahitimishwa Aprili 10.

NACTE YATANGAZA UDAHILI KWA WANAFUNZI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA NA ATASHAHADA. NACTE YATANGAZA UDAHILI KWA WANAFUNZI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA NA ATASHAHADA. Reviewed by safina radio on March 23, 2018 Rating: 5

No comments