UJERUMANI YATAKIWA KUTHIBITISHA KUWA HAITAMRESHA UHISPANIA KIONGOZI WA ZAMANI WA CATALONIA CARLES PUIGDEMONT


Mwanasheria wa kiongozi wa zamani wa jimbo la Catalonia, Carles Puigdemont, ametoa mwito kwa maafisa nchini Ujerumani kuthibitisha kwamba hawatamrejesha nchini Uhispania mwanasiasa huyo anayeshikiliwa hivi sasa nchini Ujerumani.

Image result for PICHA YA KIONGOZI WA ZAMANI WA JIMBO LA CATALONIA CARLES PUIGDEMONT
CARLES PUIGDEMONT
Mwanasheria huyo, Wolfgang Schomburg, amelieleza gazeti moja la nchini Ujerumani la the Süddeutsche Zeitung kuwa Ujerumani inapaswa kuthibitisha hatua hiyo haraka iwezekanavyo kwani vinginevyo itakuwa inaruhusu migongano ya kimaslahi ya Uhispania nchini Ujerumani.
Schomburg ambaye amewahi kuwa jaji wa mahakama ya juu nchini Ujerumani amekuwa akimwakilisha Puigdemont tangu alipotiwa mbaroni kaskazini mwa Ujerumani Jumapili iliyopita wakati alipokuwa njiani kurejea Ubeligiji akitokea Finland.

UJERUMANI YATAKIWA KUTHIBITISHA KUWA HAITAMRESHA UHISPANIA KIONGOZI WA ZAMANI WA CATALONIA CARLES PUIGDEMONT UJERUMANI YATAKIWA KUTHIBITISHA KUWA HAITAMRESHA UHISPANIA KIONGOZI WA ZAMANI WA CATALONIA CARLES PUIGDEMONT Reviewed by safina radio on March 29, 2018 Rating: 5

No comments