WAZIRI MKUU WA UINGEREZA THERESA MAY KUKUTANA NA RAIS WA UFARANSA EMMANUEL MACRON.


Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May atakutana leo na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron baada ya Ufaransa kusema ni mapema mno kuamua iwapo hatua inatakiwa kuchukuliwa kufuatia shambulizi dhidi ya jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na mtoto wake wa kike nchini Uingereza.


Image result for PICHA YA WAZIRI MKUU WA UINGEREZA THERESA MAY
WAZIRI MKUU WA UINGEREZA THERESA MAY
Ufaransa imesema leo inakubaliana na Uingereza kwamba Urusi ilihusika katika shambulizi la sumu dhidi ya jasusi wake wa zamani huko England.
Wakati haya yakiarifiwa Urusi imesema bado iko tayari kushirikiana na Uingereza kuchunguza shambulizi hilo dhidi ya afisa wake wa zamani wa ujasusi.


Image result for PICHA YA RAIS WA UFARANSA EMMANUEL MACRON
RAIS WA UFARANSA EMMANUL MACRON
Hata hivyo Uingereza imesema itawafukuza maafisa 23 wa kidiplomasia wa Urusi na kuiwekea vikwazo nchi hiyo kwa kumwekea gesi ya sumu Skripal na mtoto wake wa kike, madai ambayo Urusi inayakanusha.

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA THERESA MAY KUKUTANA NA RAIS WA UFARANSA EMMANUEL MACRON. WAZIRI MKUU WA UINGEREZA  THERESA MAY KUKUTANA NA RAIS WA UFARANSA EMMANUEL MACRON. Reviewed by safina radio on March 15, 2018 Rating: 5

No comments