DK. TIZEBA ATOA AGIZO KWA MTENDAJI MKUU WA NFRA KUNUNUA MAZAO YA WAKULIMA KWA WAKATI.


ARUSHA.

Waziri wa Kilimo hapa nchini Dk. Charles Tizeba amemwagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ghala la Chakula Nchini NFRA kuhakikisha kuwa wananunua mahindi kwa wakulima kila wanapouza mazao wanayoyahifadhi katika maghala hayo hapa nchini.

Image result for Dk. Charles Tizeba
Waziri wa kilimo Dk. Charles Tizeba.
Dk. Tizeba ametoa agizo hilo jijini Arusha wakati alipokuwa akitembelea ghala la chakula la kanda ya Arusha ambapo amesema utaratibu wa wakala kununua mahindi kwa msimu umesababisha hasara kwa kuwa hujipangia bei ya kununua.

Aidha, amesema kuwa NFRA wasisubiri mpaka msimu wa mwezi Julai kwa ajili ya kununua mazao ya wakulima kwani hali hiyo inachangia mazao ya wananchi kurundikana na kusababisha bei kushuka.

Pia, ameitaka Wakala hao kuondokana na utaratibu huo wa kusubiri muda Fulani ili kununu mahindi bali wanunue mahindi wakati wowote pamoja na kuhakiki mazao hayo ili kubaini kasoro zilizopo.

Hata hivyo Waziri Tizeba ametumia nafasi hiyo kuwatahadharisha wakuu wote wanaosimamia Maghala ya Chakula ya Taifa kuwa yeyote atakaye zembea kuuza mazao ya chakula aliyonayo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

DK. TIZEBA ATOA AGIZO KWA MTENDAJI MKUU WA NFRA KUNUNUA MAZAO YA WAKULIMA KWA WAKATI. DK. TIZEBA ATOA AGIZO KWA MTENDAJI MKUU WA NFRA KUNUNUA MAZAO YA WAKULIMA KWA WAKATI. Reviewed by safina radio on March 15, 2018 Rating: 5

No comments