SHAMBULIZI LASABABISHA VIFO VYA WATU 37 MASHARIKI MWA GHOUTA.
Mashambulizi yanayoendelea kufanywa na
jeshi la Assad mashariki mwa ghouta yamesababisha vifo vya watu 37 na
wengine kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa habari,raia 37 wakiwemo wanawake na watoto wamepoteza maisha kwa kuunguzwa na mabomu yaliyorushwa na Assad katika amshambulizi hayo.
Jeshi la Assad limekuwa likishirikiana na
Urusi kufanya mashambulizi hayo nchini Syria.
Ripoti zinaonesha kuwa idadi ya vifo
inaweza kuwa kubwa zaidi kwani mashambulizi bado hayajasitishwa.
Licha ya Umoja wa Mataifa kuitaka Syria
kuachana na mashambulizi hayo,jeshi la Assad linaonekana kutokuwa na nia ya
kufuata maagizo hayo.
SHAMBULIZI LASABABISHA VIFO VYA WATU 37 MASHARIKI MWA GHOUTA.
Reviewed by safina radio
on
March 23, 2018
Rating:

No comments