RAIS MAGUFULI AZINDUA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA RELI YA KATI YA MWENDO KASI YA STANDARD GAURGE.


DODOMA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli amezindua jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kati ya mwendo kasi ya Standard Gaurge inayotoka Matoporwa-Morogoro hadi Ihumwa mkoani Dodoma.

Image result for Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kiseikali kutoka ndani na nje ya nchi, Rais Magufuli amesema kuwa mradi huo wa awamu ya pili unagharamiwa kwa fedha za watanzania kwa zaidi ya shilingi trilioni 7.

Aidha, amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kuwaajiri watanzania zaidi ya elfu thelathini kuwa wafanyakazi wa kudumu na wafanyakazi elfu sita wasio wa kudumu katika kutekeleza mradi huo.

Pia, amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imejibu suala la ajira kwa vitendo ambapo ameelezea miradi mbali mbali mikubwa iliyoanzishwa na serikali katika kuleta maendeleo ya nchi ikiwemo mradi wa umeme wa Stilllers George, usambazaji wa umeme vijijini- REA, na kutengenezwa kwa Meli kubwa katika ziwa Victoria.

Hata hivyo, amewataka wananchi kuwa wazalendo katika kulipa kodi ili kuharakisha maendeleo ya nchi huku akiitaka Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi Tanzania-TRA kuhakikisha kuwa inatoa elimu kwa wananchi kwa ajili ya kuondoa tabia ya ukwepaji wa malipo ya kodi.  

RAIS MAGUFULI AZINDUA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA RELI YA KATI YA MWENDO KASI YA STANDARD GAURGE. RAIS MAGUFULI AZINDUA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA RELI YA KATI YA MWENDO KASI YA STANDARD GAURGE. Reviewed by safina radio on March 14, 2018 Rating: 5

No comments