TRUMP AMPONGEZA PUTIN

Rais wa Marekani Donald Trump amempongeza Rais wa Urusi Vladmir Putin kwa kushinda muhula wa nne madarakani katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita.

Image result for PICHA YA TRUMP
RAIS TRUMP

Trump amesema amempigia simu Putin kumpongeza kwa ushindi huo na pia kujadili uwezekano wa kuandaa mkutano wa kilele kati yao katika siku za hivi karibuni.

Viongozi hao wawili pia wamejadili umuhimu wa kuwa na juhudi za pamoja za kupunguza ushindani wa kuoneshana nguvu za kijeshi, kuimarisha uchumi, mizozo ya Ukraine na Syria na pia wamejadili mpango wa kinyuklia wa Korea Kaskazini.

Hata hivyo hawakujadili suala la Urusi kudaiwa kuhusika katika kumshambulia Sergei Skripal, jasusi wa zamani wa Urusi anayeishi Uingereza ambapo Nchi za magharibi zimeghadhabishwa na shambulizi hilo la kutumia silaha za sumu.

Naye Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un pia amempongeza Rais Putin na kumtakia kila la kheri katika kulijenga taifa lenye nguvu zaidi.
TRUMP AMPONGEZA PUTIN TRUMP AMPONGEZA PUTIN Reviewed by safina radio on March 21, 2018 Rating: 5

No comments