UN YAONGEZEA MUDA UNMISS, SUDAN KUSINI.


JUBA.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha uamuzi wa kuiongezea muda tume maalumu ya Umoja huo nchini Sudan Kusini UN MISS hadi tarehe 15, Machi mwakani katika zoezi la kutokomesha vita nchini humo.

Image result for Sudan Kusini UNMISS
Walinda amani katika ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS.

Uamuzi huo umezitaka pande mbalimbali za Sudan Kusini zisimamishe vita mara moja, na kusema kuwa baraza la usalama litafikiri kuchukua hatua zote na kuwaadhibu watu wanaovuruga amani, utulivu na usalama wa Sudan Kusini.

Habari zinaeleza kuwa uamuzi huo pia umeamua kudumisha ukubwa wa tume hiyo iliyo na askari wasiozidi elfu kumi na saba na polisi elfu mbili mia moja na moja.

Askari hao watakuwa pamoja na wale wa kikosi cha ulinzi cha kikanda kitakachoundwa chini ya idhini ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, lakini hakitakuwa na askari zaidi ya elfu 4.


UN YAONGEZEA MUDA UNMISS, SUDAN KUSINI. UN YAONGEZEA MUDA UNMISS, SUDAN KUSINI. Reviewed by safina radio on March 16, 2018 Rating: 5

No comments