IMEBAINISHWA KUNA UMUHIMU WA KUFANYA UKOMBOZI WA KISIGINO
Imebainishwa kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kila mtu
kufanya ukombozi wa kisigino chake kwakuwa adui amekuwa akitumia kisigino cha
mguu wa mtu kuharibu kusudi la Mungu na kumfanya kupoteza muelekeo wa maisha.
Huduma ya redio safina kesho katika ukumbi wa maombi
uliopo mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana imekuandalia
maombi maalumu ya mwendelezo wa kuchovya miguu kwenye mafuta pamoja na
kuwaombea watoto ili Mungu aweze kuwaweka mbali na vifungo malimbali katika
maisha yao.
Aidha kwa mujibu wa somo hilo wapo watu ambao
wameendelea kutaabika na magonjwa,kutokupata kazi hatakama wamesoma,migogoro
katika ndoa,kukosa watoto,mimba kuharibika au kupata watoto wa jinsia moja kutokana
na adui kukamata visigino vya miguu na kuharibu misingi ya maisha yao.
Vile live katika maombi hayo ya mwendelezo wa
kuchovya miguu kwenye mafuta pia kutafanyika maombi kwaajili ya watoto ambao ni
wakorofi wasio wasikiliza wazazi wavuta bangi,wezi,watoto wasiopenda kwenda
shule pamoja na watoto wachanga ambao wanalia nyakati za usiku.
Hata hivyo kesho katika ukumbi wa maombi wa safina
redio uliopo mbauda jijini Arusha kila atapaswa kuja na kitambaa kwaajili ya
kufanya kitendo cha imani.
IMEBAINISHWA KUNA UMUHIMU WA KUFANYA UKOMBOZI WA KISIGINO
Reviewed by safina radio
on
March 19, 2018
Rating:
No comments