DK. TIZEBA AMUAGIZA MRAJISI MSAIDIZI WA NCU KILIMANJARO KUWASILISHA MIKATABA YA WAWEKEZAJI KATIKA SHAMBA LA LA KIBO AND KIKAFU ESTATE.
KILIMANJARO.
Waziri wa Kilimo Hapa nchini Dk. Charles Tizeba
amemwagiza Mrajisi Msaidizi wa ushirika Mkoani Kilimanjaro kuwasilisha mikataba
ya wawekezaji katika Shamba la Kibo and Kikafu Estate lililopo wilayani Hai
mkoani humo.
Waziri wa KilimoDk. Charles Tizeba. |
Akizungumza mkoani humo wakati alipomtembelea
mwekezaji huyo Dk. Tizeba amesema kuwa hawezi kumvumilia mwekezaji asiyekuwa na
Mkataba wa Uwekezaji.
Waziri huyo ametaka suala hilo lifanyike mara moja
licha ya muda waliyojiwekea huku akisema
kuwa mtu hawezi kuwekeza fedha mahali ambapo hana mkataba nakumtaka mwekezaji
huyo kupeleka mkataba wake na sambamba na mkataba wa mwekezaji wa kwanza.
Naye Mwekezaji wa Shamba hilo Shrevod Givodi amesema
kuwa ameshindwa kuwa na mkataba kutokana na kushindwa kupata muafaka katika
majadiliano na ofisi ya mkoaa na mwekezaji aliyeondoka.
Vile vile, Dk. Tizeba ametembelea mashamba ya kahawa
ya Kilimanjaro Plantation na Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro NCU.
DK. TIZEBA AMUAGIZA MRAJISI MSAIDIZI WA NCU KILIMANJARO KUWASILISHA MIKATABA YA WAWEKEZAJI KATIKA SHAMBA LA LA KIBO AND KIKAFU ESTATE.
Reviewed by safina radio
on
March 14, 2018
Rating:
No comments