WATU 47 NCHINI CONGO DRC WAMEUAWA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA KATIKA MAANDAMANO.

Image result for PICHA YA ZEID RA'AD AL HUSSEIN
Zeid Ra'ad Al Hussein

Ripoti ya umoja wa Mataifa imeonesha kuwa jumla ya raia 47 wameuawa katika kipindi cha mwaka mmoja wakati vyombo vya usalama vya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo vilipokabiliana na waandamanaji wanaopinga utawala wa rais Joseph Kabila.
Sehemu ya ripoti hiyo imedai kuwa kati ya Januari Mosi mwaka 2017 hadi Januari 31 mwaka 2018, watu 47 wakiwemo wanawake na watoto waliuawa na vyombo vya usalama wakati wa maandamano.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa kulikuwa na jaribio lililofanywa na vyombo vya usalama vya DRC kutaka kufunika na kuficha ukweli kuhusu vifo hivi kwa kuondoa miili na kuzuia kazi za waangalizi wa kimataifa.
Ripoti hiyo ilivyochapishwa na mkuu wa tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa na tume ya umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, Zeid Ra'ad Al Hussein na mjumbe maalumu wa UN Leila Zerrougui wamesema mauaji na vitendo vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilitekelezwa kutokana na matumizi makubwa ya nguvu yaliyofanywa na vyombo vya usalama dhidi ya waandamanaji.
Umoja wa Mataifa unalaani ukandamizaji wa kupangwa dhidi ya waandamanaji ikiwemo kutumia njia za mateso dhidi ya waandamanaji jambo ambalo linaenda kinyume na sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu pamoja na zile sheria za DRC.

WATU 47 NCHINI CONGO DRC WAMEUAWA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA KATIKA MAANDAMANO. WATU 47 NCHINI CONGO DRC WAMEUAWA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA KATIKA MAANDAMANO. Reviewed by safina radio on March 20, 2018 Rating: 5

No comments