VALDS DOMBROVSK AAHIDI KUIPA USHIRIKIANO UINGERERA DHIDI YA SHAMBULIZI LA SUMU KWA JASUSI WA ZAMANI WA URUSI.
BRUSSELS.
Umoja
wa Ulaya umeahidi kuipa ushirikiano Uingereza kufuatia nchi hiyo kuituhumu
Urusi kuhusika na shambulizi la sumu dhidi ya jasusi wa zamani wa Urusi pamoja
na binti yake.
Ahadi
hiyo inakuja baada ya kutolewa na makamu wa rais wa halmashauri ya Ulaya Valdis
Dombrovskis wakati kukiwa na wasiwasi nchini Uingereza kuhusu ushirikiano wa
kiusalama baada ya nchi hiyo kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya mwishoni mwa Machi
2017.
Makamu wa rais wa halmashauri ya Ulaya Valdis Dombrovskis. |
Naye
msemaji wa mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Federeca Moghereni amelielezea
shirika la habari la Reuters kuwa matumizi ya silaha za sumu katika jaribio la
kuwaua raia nchini Uingereza ni suala linaloshtua.
Hata
hivyo, ameongeza kuwa Umoja wa Ulaya unaungana na Uingereza katika kuhakikisha
kuwa haki inapatikana pamoja na kuahidi kutoa ushirikiano itakapolazimu kutoa
ushirikiano dhidi ya uchunguzi huo.
VALDS DOMBROVSK AAHIDI KUIPA USHIRIKIANO UINGERERA DHIDI YA SHAMBULIZI LA SUMU KWA JASUSI WA ZAMANI WA URUSI.
Reviewed by safina radio
on
March 14, 2018
Rating:
No comments